The House of Favourite Newspapers

SIKIA MAPYA YA ZARI, MOND KUHUSU NDOA

Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’

DAR ES SALAAM: Tambo! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mastaa ‘zilipendwa’; Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuonekana kurushiana jumbe tofauti za kuonesha kila mmoja anataka kuingia kwenye ndoa na mtu tofauti.  

 

Baada ya kumwagana mapema mwaka huu na ukimya mrefu kupita, Diamond ndiye aliyekuwa wa kwanza kuonesha tambo hizo baada ya kutangaza kuwa atamuona mwanadada kutoka Kenya, Tanasha Donna Barbieri Okech ‘Zahara Zaire.’

 

Diamond alitoa kauli hiyo alipokuwa kwenye Tamasha la Wasafi hivi karibuni pande za Mtwara ambapo alidai kuwa, atamuoa mrembo huyo Februari 14, mwakani. Siku chache baadaye, Zari ambaye amezaa na Diamond watoto wawili kabla ya kuachana, naye ametupia ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram ulioshiria kujibu mapigo hayo kwa kusema anatamani kuolewa na mwanaume ambaye atawajali watoto wake.

Kwenye posti hiyo, Zari alikopi ujumbe uliokuwa ukiwahamasisha akina mama wanaowalea watoto peke yao (single mothers) kuwa makini katika kuchagua wanaume wa kuwaoa, ambao wataweza kuwahudumia watoto, kisha akasindikiza na ujumbe wake uliosomeka hivi:

 

“Nimekuwa kwenye mahusiano kadhaa baada ya ua rose jeusi lakini anayefuata naamini atakuwa baba bora. Baba ambaye atawajali watoto wangu wa kiume pamoja na binti yangu, naamini siku moja nitampata mwanaume wa hivyo,” aliandika Zari kwa lugha ya Kingereza.

 

Zari alitangaza kumuacha Diamond Februari 14, mwaka huu kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka ua rose jeusi kisha kusindikiza na ujumbe wa kumuacha baba watoto wake huyo kwa madai ya kuwa amezidisha michepuko.

Stori: Mwandishi Wetu, Ijumaa

Comments are closed.