The House of Favourite Newspapers

SIKU 3 ZA PAPARAZI NDANI YA DANGURO!

DANGURO moja maarufu lililopo Sinza Mori jijini Dar, licha ya mara kadhaa kikosi cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kulifungia kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, bado limeendelea kufanya kazi zake na safari hii mwandishi wetu ameweka kambi kwa saa 72 na kubaini uozo wa kutisha.

 

LIKO ENEO GANI?

Danguro hilo lipo Sinza Mori jijini Dar, barabara ya kuelekea Meeda upande wa kulia ambapo zamani palikuwa na gesti, baadaye jengo likabadilishwa na kuwa la kampuni kabla ya kubainika kuwa, bado shughuli za wanawake kujiuza ndani ya jengo hilo zinaendelea.

 

Siku za hivi karibuni, gazeti ndugu na hili la Risasi Mchanganyiko lilitoa habari za jengo hilo lenye vyumba takribani 20 kutumika kama danguro licha ya getini kuwepo kwa maneno yanayoonesha ni jengo la kampuni. Baada ya habari hiyo kuandikwa, inadaiwa mmiliki wa jengo hilo aliamuru maandishi yaliyo getini yafutwe kisha kuzuia akinadada wanaotumia vyumba vilivyomo ndani ya jengo hilo kujiuza kuacha ili kuepuka mkono wa sheria.

BIASHARA YAFUNGWA KWA MUDA

Kufuatia kuandikwa kwa habari hizo, biashara ya wanawake kujiuza ndani ya danguro hilo ilisitishwa ambapo mwandishi wetu alifika na kubaini vyumba vingi vimefungwa na hata waliokuwa wakionekana eneo hilo hawakuwa tayari kutoa huduma ya ngono.

Msichana mmoja aliyekutwa eneo hilo saa 8 mchana alidhihirisha biashara ya kujiuza eneo hilo kuingia ‘mdudu’ akisema; ‘Ukitaka labda twende sehemu nyingine, humu sasa hivi ni ngumu.’

Paparazi: Ugumu unakujaje, si tunaingia mara moja tu nakupa chako.

Dadapoa: Sasa hivi polisi hawakauki hapa, si unaona vyumba vingi vimefungwa? Kama unataka twende kuna gesti iko kwa mbele hapo. Kufuatia maneno ya msichana huyo, paparazi wetu aliondoka akiwa amejiridhisha kuwa, habari iliyoandikwa na Gazeti la Risasi ilizaa matunda.

WIKI MBILI BAADAYE, BIASHARA KAMA KAWAIDA

Baada ya kupita kama wiki mbili hivi, mmoja wa wakazi wa eneo hilo alipiga simu na kueleza kuwa, biashara ya ngono ndani ya jengo hilo imerejea kama kawaida na usumbufu umekuwa ‘kama wote’. “Sasa hivi huduma kama kawaida, jengo limefurika akinadada tena wale waliofungashia tu, yaani sijui anayemiliki jengo lile ni nani na analindwa na nani,” alisema raia huyo mwema aliyegoma kutaja jina lake.

Katika kufuatilia ili kujua kama biashara hiyo imerejea ndani ya jengo hilo ambalo kwa nje huwezi kuamini kama ndani yake kuna ufirauni unafanyika, mwandishi wetu Oktoba 13, mwaka huu saa 8 mchana alitinga eneo hilo na kukuta takribani vyumba 10, mlangoni kuna akinadada waliokuwa wamefunga kanga moja kuashiria ni wewe tu na pochi yako.

Mwandishi wetu baada ya kuona hali hiyo, alimfuata dada mmoja aliyeonekana kumuita kiaina na alipomkaribia mazungumzo yalikuwa hivi:

Dadapoa: Karibu baby, ‘short time’ elfu kumi.

Paparazi: Mimi na buku tano tu.

Dadapoa: (huku akimvutia ndani paparazi), acha ubahili wewe, buku tano ndiyo nini? Hapa ni kuanzia elfu kumi, hata nikikuachia hakuna mwanamke wa kukupa huduma ya elfu tano humu ndani.

Paparazi: Ndo’ ninayo hiyo tu sasa.

Dadapoa: Sikia, elfu tano ndiyo yangu, elfu tano nalipia chumba, ndiyo maana nakuambia unipe elfu kumi. Acha ubahili wee kaka, toa pesa utafurahi na roho yako.

Papapazi: Basi ngoja nitoke, narudi.

 

Baada ya paparazi kutoka nje, akakumbana na mrembo mwingine ambaye bila kujua paparazi huyo kashindwana bei na mwenzake, naye alimvutia huku akimwambia: “Njoo huku wewee”.

Kwa kuwa mwandishi alikuwa kazini, hakuonesha kukataa, fumba na kufumbua alijikuta kwenye chumba chenye kitanda cha sita kwa sita, mezani kukiwa na boksi la kondomu.

Dadapoa: Sema mpenzi, nikuhudumie nini?

 

Paparazi: Kwani shilingi ngapi?

Dadapoa: Unalipia chumba elfu 5, mimi unanipa elfu 10 kwa short time, kama unataka uwe mume wangu kuanzia muda huu hadi asubuhi, nipe elfu 50. Utasahau shida zako zote.

Paparazi: Elfu 50, mbona nyingi?

Dadapoa: Kama nyingi basi nenda kwa mkeo.

 

Paparazi: Basi nakuja tulale hadi asubuhi.

Dadapoa: Poa.

Baada ya makubaliano hayo, paparazi wetu akatoka nje na kukuta muda huo wa saa 11:15 jioni wanaume walikuwa wakipishana kuingia kwenye vyumba.

Je, siku hiyo paparazi alirudi kwenye danguro hilo? Je, mfumo wa biashara ya ngono katika eneo hilo ukoje? Fuatilia Jumanne ijayo kwenye gazeti hilihili.

Comments are closed.