Silaha 4 Yanga zampa kiburi Zahera

Uwepo wa washambuliaji wanne pale Yanga umeonekana utampa kiburi Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ambaye msimu uliopita alionekana kumtegemea zaidi straika Heritier Makambo ambaye amesepa.

 

Katika usajili mpya Yanga ina uwezo wa kuwachezesha katika nafasi hiyo nyota wake Juma Balinya, Mzambia Maybin Kalengo, Mnyarwanda Issa Bigrimana, Mnamibia Sadney Urikhob na Patrick Sibomana raia wa Rwanda. Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila alisema kwa kiasi fulani sasa presha kwenye eneo la ushambuliaji na mabeki imepungua na mashabiki watanogewa msimu ujao.

“Nafurahishwa na uwepo wa mastraika wengi kikosini kwani siku zote huwezi kusema una kikosi kizuri kama hujajitosheleza katika kila nafasi kama walau ilivyo kwa sasa ambapo utaona washambuliaji tu pekee wapo zaidi ya wanne.

 

“Lakini hata kwa sasa ukizungumzia kikosi kwa ujumla utagundua hakuna sana presha kama tuliyopitia msimu uliopita ambapo ilikuwa ukimkosa mchezaji fulani lazima uwe na mawazo kama sasa ukiwaza straika utamuona Balinya, Kalengo, Sadney na Bigrimana hiyo inaenda hivyo hadi kwa mabeki na viungo,” alisema Mwandila


Loading...

Toa comment