The House of Favourite Newspapers

SILAHA MUHIMU ZA KUMFANYA AFURAHI MUWAPO FARAGHA

Picha inayohusiana

TENDO la ndoa (kwa wanan­doa) si tu linatumika kubore­sha uhusiano kati ya mume na mke bali pia ni dawa inay­oweza kuutibu mwili, akili na hisia. Hata hivyo, lazima liwe ni tendo lililokamilika, kwa maana lazima mwanaume na mwanamke wote walifurahie na kuridhika.

Tendo hili lisipofanyika kwa ukamilifu wake, hubadilika na kuwa kero kubwa na janga kwa wanandoa. Kama ambavyo nimekuwa nikieleza mara kwa mara, sidhani kama yupo mtu ambaye hataki kumfurahisha mwenzi wake wawapo faragha. Tatizo ni kwamba wengi hawana maarifa ya nini cha kufanya awapo fara­gha na mwenzi wake, na matokeo yake wamekuwa wakijiendea wanavyoweza, kama kutembea kwenye giza totoro usiku wa manane.

Hakuna mahali ambapo unaweza kufundishwa namna ya kumfurahisha mumeo au mkeo, angalau kidogo wazee wetu enzi zao walikuwa wanapelekwa jan­doni na unyagoni, siku hizi unakuja kujifunzia ndani ya ndoa, yaani kama ni mechi ya mpira wa miguu basi unajifunzia kutuliza mpira na kupiga danadana uwanjani wakati wa mechi ambayo ni lazima ushinde.

Mfano mwepesi ambao huwa napenda kuutu­mia ni kwamba kila mtu anaweza kuwa anatamani kupiga gitaa na kuzalisha muziki mzuri, lakini hebu jiulize, kama hujawahi kujifunza kupiga gi­taa na ukaelewa, ukipewa gitaa sasa hivi unaweza kupiga na kutoa muziki mzuri? Jibu ni HAPANA.

Mapenzi ni sanaa, kwa hiyo lazima ukubali kujifunza na kuyatafuta maarifa mahali popote yalipo ili uwe bora, huyo uliyenaye unaweza kuwa unafanya kila kitu kwa ajili yake, unajita­hidi kumuonesha upendo wa hali ya juu lakini kama hujui nini cha kufanya muwapo faragha ili afurahi, ni sawa na kazi bure. Ni kwa msingi huo ndiyo maana nikaamua tujadiliane mada hii kama inavyojieleza hapo juu.Picha inayohusiana

MAANDALIZI YA KIHISIA

Jambo la kwanza ambalo unatakiwa kulifaha­mu, ni kwamba ili mume au mke afurahie tendo muwapo faragha, lazima awe ametulia kihisia. Haiwezekani mmetoka kukwazana kuhusu jambo fulani, hamjapata suluhu na kila mmoja ana hasira halafu ndiyo mnaingia uwanjani, hamuwezi kufurahia tendo kwa mtindo huo na hii inawahusu wote.

Maandalizi mazuri ya tendo yanaanzia katika maelewano, mpokee vizuri kwa maneno yaliyo­jaa bashasha, kwa sauti ya upole, mbembeleze, mpetipeti na msifie! Ukiikamilisha kwa uka­milifu hatua hii ya kwanza na ya muhimu, basi utakuwa tayari umeshamuingiza kwenye safari ya kuelekea kufurahia tendo.

Mnapokuwa eneo la tukio, hutakiwi kuwa na papara! Lazima kwanza na wewe akili yako uitulize na badala ya kukimbilia kuingia mchezoni na kuanza kupiga mbizi kama mtu anayejifunza kuogelea, unatakiwa kwanza kutumia muda wa kutosha kupasha misuli moto.Tokeo la picha la BLACK COUPLES ON BED

Muda unaoshauriwa kitaalamu, ni angalau dakika thelathini, ndani ya muda huu mfanyie yale mambo yatakayoamsha hisia zake za ndani, viungo vya mwili wako kama mikono, vidole, mdomo, masikio vinaweza kuzalisha hisia nzuri sana kama utakuwa unajua nini unatakiwa kufanya kwa wakati gani.

Narudia tena, epuka kuwa na papara za kukimbilia uwanjani, maandalizi ni muhimu sana kwani yatamuandaa mwenzi wako kimwili na kihisia. Ukiwa na uhakika kwamba maandalizi yamefanyika kwa ukamilifu, sasa unaruhusiwa kuendelea na hatua kubwa na ya muhimu inayofuatia.

Katika hatua hii ambayo kimsingi ndiyo inayowaun­ganisha, pia unatakiwa kuwa na uelewa juu ya nini cha kufanya na kwa mtindo gani, siyo unaingia kwa papara kama unakimbizwa, hapana. Hapa pia unatakiwa kujifunza zaidi ili kuhakikisha unaibuka mshindi kwa kumfikisha mwenzi wako kwenye kilele cha safari yake ya huba.Kwa leo tuishie hapa, tutaen­delea wiki ijayo sehemu ya pili.

Comments are closed.