The House of Favourite Newspapers

SIMANZI NA MAJONZI KUAGWA MWILI WA MAMA WA SHIGONGO – VIDEO

Watawa wa Kanisa Katoliki alilokuwa akisali marehemu wakiaga mwili.

SIMANZI, majonzi vimetawala wakati wa kauagwa kwa mwili wa mama mzazi wa Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, Bi. Astreia Kahabi Kapela nyumbani kwake maeneo ya Mikocheni B, jijini Dar es Salaam leo Julai 29, 2018.

Waandishi wa Habari wa Global Publishers, Martha Mboma, Imelda Mtema na Katibu Tawala wa Ilala, Edward Mpogolo wakaiaga mwili.

Bi. Asteriua Kapela alifariki dunia alfajiri ya Ijumaa, JulaiĀ  27 mwaka huu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Baada ya kuagwa leo nyumbani kwake, mwili wa marehemu umepelekwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Agatha lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam kwa ajili ya iabada ya kumwombea marehemu kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Mwanza kwa mazishi.

Mhariri wa Gazeti la Championi, John Joseph akiaga mwili.
Mwanafamilia, Mariam (mbele), na wafanyakazi wa Global Publishers, Glory Lucas, Diana na Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Spoti Xtra, Samson Mfalila wakitoa heshima zao za mwisho.
Mjukuu wa Maerehemu na Mhariri wa Championi, Ezekiel Kitula akiaga.
Watangazaji wa Global TV, Catherine Kahabi, Mpanga na wenzao wakiaga.
Mwandishi wa Global, Andrew Carlos akiaga.
Mfanyakazi wa Global, Huruma Bujiku akiaga.
Mwanasheria wa Global Publishers, Emmanuel Elias akitoa heshima za mwisho.
Mjukuu mkubwa wa marehemu, James Bukumbi akiaga.
Mjukuu wa marehemu, Kulwa Bukumbi akiaga.
Mtoto mkubwa wa marehemu, Leah James Bukumbi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mama yake.
Mtoto wa Marehemu ambaye pia ni MKurugenzi wa Global Publishers, Lydia James Bukumbi akilia wakati wa kuaga mwili wa mama yake.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Eng. James Kilaba akitoa heshima za mwisho.
Mtoto wa Marerhemu, Marsha James Bukumbi akitoa heshima za mwisho kwa mama yake.
Shigongo akitoa heshima za mwisho kwa mama yake.
Shigongo na mkewe, Veneranda Ephraim baada ya kuaga,.
Mwili wqa marehemu ukipandishwa kwenye gari kwa ajili ya kuelekea kanisani.

PICHA NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

 

VIDEO: SHUHUDIA TUKIO LA KUAGWA MWILI WA MAMA WA HSHIGONGO

Comments are closed.