The House of Favourite Newspapers

Simanzi, Vilio Vyatawala Mazishi ya Watoto Waliolipukiwa na Bomu Monduli

0
Watoto wakibeba jeneza lenye mwili wa mwenzao, Johnson Daniel.

NI SIMANZI na vilio vimetawala  katika Kijiji cha Nafco Kata ya Loksale, wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maziko ya watoto watatu waliopoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu wakichunga mifugo ya familia kwenye eneo la mafunzo ya jeshi la Loksale wilayani hapa Ijumaa iliyopita.

 

Mama mzazi wa marehemu Jonsoni akiweka mchanga kwenye kaburi la mwanaye.

Katika mazishi hayo, viongozi wa Jeshi na Serikali wametoa tahadhari kwa wananchi wanapofanya shughuli kwenye maeneo yanayotumika kwa mafunzo ya kijeshi.

Simanzi, Vilio Vyatawala Mazishi ya Watoto Waliolipukiwa na Bomu Monduli

 

Miili ya marehemu ikipelekwa makaburini.

Watoto hao, Johnson Daniel Mollel, mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Nafco akiwa na wenzake Emmanuel Saitabau Mollel wa darasa la kwanza na Samweli Nyangusi Laizer walipoteza maisha wakati wakichunga baada ya kulipukiwa na bomu.

 

Wanafunzi wakiwa wamejipanga kupokea miili ya wenzao.

Brigedia Jenerali Rajab Hunt kutoka Kambi ya Monduli amesema tukio hilo halikutarajiwa kwa kuwa Serikali inanunua silaha kwa ajili ya ulinzi na si kuwadhuru wananchi.

 

​Mkuu wa Wilaya ya Monduli Bw. Idd Hassan Kimanta akiaga miili ya marehemu.

“Eneo letu tunalolitumia kwa mafunzo ni kubwa wakati mwingine mabomu hayalipuki kutokana na umri wake au namna lilivyotengenezwa linachukua muda kulipuka, hivyo niwaombe wananchi mnapoona vitu mnavyokuwa na shaka navyo toeni taarifa kambini tutawatuma wataalamu kuja kuyategua,” alisema Brigedia Hunt

 

DC Kimanta akitoa pole kwa wafiwa.​

Akizungumzia hilo, Mkuu wa Brigade ya Mbuni, Brigedia Jenerali Athanas Mbonye amesema wananchi wasiwe na wasiwasi kwa sababu jeshi lipo kuwalinda na watoe taarifa wanapoona vifaa wanavyovitilia shaka.

 

Amewataka wazazi kuwaelimisha watoto namna ya kuchukua tahadhari wanapokuwa machungani kwenye maeneo ya jeshi.

JWTZ Wakizika Miili ya Watoto Waliolipukiwa Bomu Monduli

Simanzi ikitawala.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta amewataka wananchi wanaochunga mifugo eneo linalotumika kwa mafunzo ya kijeshi kutoa taarifa kwenye kambi za jeshi ili kuepusha madhara ya vifo.

 

 

Viongozi wa jeshi na wa serikali wakiwa msibani hapo.

 

Amesema kwa muda mrefu kumekuwa na ushirikiano kati ya kambi za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zilizopo wilayani humo na vijiji vinavyozunguka maeneo ya mafunzo, hivyo tukio hilo ni la bahati mbaya.

Ibada ya kuaga.

 

“Wakati tukio hili likitokea nilikuwa kwenye mahafali ya kuhitimu vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya Makuyuni. Kwa kushirikiana na maofisa wa jeshi tulifika eneo la tukio na kuifikisha miili kwenye hospitali ya wilaya kuihifadhi,” amesema Kimanta.

Kiongozi wa mila wa jamii hiyo ya wafugaji, Loibanguti Loondawa alisema tukio hilo limeleta majonzi kwa familia na ni la bahati mbaya kwa kuwa halikuwa limekusudiwa.

NA HIULALY DAUDI | GPL

Leave A Reply