The House of Favourite Newspapers

FT FA CUP: Simba SC 1-0 Azam FC Kutoka Uwanja wa Taifa

0

Dakika ya 98: Mchezo unaendelea baada ya kipa kusimama na kuendelea na mchezo.

Dakika ya 96: Mchezo bado umesimama kipa anatibiwa.

Dakika ya 93: Azama wanafanya shambulizi langoni mwa Simba lakini mpira unatoka, wachezaji na benchi la ufundi la Azam wanalalamikia mchezaji wao kachezewa faulo na ilitakiwa penati.

Dakika ya 91: Simba wanafanya,mabadiliko, anatola Ibrahim Ajibu, anaingia Blagnoun.

Dakika ya 90; Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 5 za nyongeza. Mabadiliko ya Simba yanaonekana kuamsha hamsa kwa kikosi cha Simba kinacheza vizuri.

Dakika ya 88: Simba wanamtoa Kotei, anaingia Said Ndemla, mchezo sasa umebalansi pande zote zikishambuliana kwa zamu.

Dakika ya 86: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mavugo, anaingia Mwinyi Kazimoto.

Dakika ya 84: Bocco anakosa nafasi, anapiga kichwa kipa wa Simba akiwa ameshatoka langoni,Boukungu anauwahi mpira na kuupiga mbali na lango. Kumbuka kuwa timu zote sasa zina wachezaji 10 uwanjani kila upande.

Dakika ya 82: Azam wanafanya mabadiliko, anatoka Singano, anaingia Mudhathir Yahaya.

Dakika ya 76: Mohamed Ibrahim ‘Mo’ anatolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na faulo hiyo aliyomchezea Kapombe.

Dakika ya 76: Mchezo umesimama baada ya Mohamed Mo kumchezea faulo Kapombe wakati akiwania mpira, Kapombe anatimbiwa kwa muda.

Dakika ya 73: Mkude anamchezea faulo Singano nje kidogo ya lango la Simba, mwamuzi anaweka ipigwe faulo. inapigwa kipa wa Simba anadaka.

Dakika ya 72: Kasi ya mchezo imepungua kiasi, ghafla Simba wanafika kwenye lango la Azama lakii Mavugo anashindwa kumalizia kazi kwa kuwa mpira umekuwa juu.

Dakika ya 69: Wachezaji wa Azam wanagongana kichwani wakti wakiwania mpira, Singano anaumia na mwamuzi anasimamisha mchezo kwa sekunde kadhaa kisha unaendelea.

Dakika ya 60: Azam wanafanya mabadiliko anaingia Joseph Mahundi.

Dakika ya 58: Simba wanaonekana kujipanga, wanapiga pasi nyingi za uhakika, wanatengeneza nafasi.

Dakika ya 52: Beki wa Azam, Agrey Morris anapiga kichwa langoni mwa Simba lakini mpira unapaa juu.

Dakika ya 51: Azam nao wanajibu mashambulizi kwa kusogea kwenye lango la Simba.

Mavugo aliingia na mpira kutoa upande wa kulia, akapiga krosi nzuri ambayo ilitua kwa mfungaji, aliyekuwa amesimama peke yake, akaupiga mpira kwa shuti kali, lililodunda na kuingia wavuni.

Dakika ya 48: Simba wanapata bao la kwanza likifungwa na Mohamed Ibrahim ambaye amemalizia kazi nzuri ya Mavugo.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!

Dakika ya 47: Mchezo umeanza taratibu, kasi inaanza kuwa kubwa taratibu, Simba wameshafika langoni mwa  Azam mara moja.

Wakati timu zinaingia uwanjani, Azam FC ilifanya mabadiliko, ilimtoa Shaban Idd na nafasi yake ikachukuliwa na Frank Domayo.

Kipindi cha pili kimeanza. Mwamuzi amepuliza kipenga kuendeleza mchezo huu wa nusu fainali ya Kombe la FA, matokeo bado ni 0-0.

Muda wowote kuanzia sasa kipindi cha pili kitaanza.

Timu zinarejea uwanjani, waamuzi wameshafika katikati ya uwanja.

MAPUMZIKO: SIMBA 0-0 AZAM FC

Dakika ya 48: Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza, lakini wachezaji wa Azam wanamfuata mwamuzi wakimlalamikia.

Dakika ya 47: Inapigwa faulo kuelekea langoni mwa Simba lakini Juuko Murshid anamdhibiti John Bocco na anaokoa.

Dakika ya 45: Shomari Kapombe yupo chini baada ya kuchezewa faulo. Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

Dakika ya 44: Simba wanafanya shambulizi kali, wanagongeana vizuri lakini akiwa ndani ya eneo la 18, Ajibu anapiga shuti linalotoka nje ya lango.

Dakika ya 41: Kichuya anawatoka walinzi wa Azam lakini mpira unakuwa na kasi kubwa, kipa wa Azam, Aishi anauwahi na kuudaka.

Dakika ya 40: Straika wa Simba, Laudit Mavugo anamchezea faulo beki wa Azam ndani ya eneo la 18 la Azam wakati wakiwania mpira na mwamuzi anapuliza kipenga.

Dakika ya 39: Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ anaunawa mpira na inakuwa faulo kuelekea Simba.

Dakika ya 35: Mchezo unaendelea kwa kasi huku mvua ikinyesha lakini hiyo haipunguzi kelele za mashabiki hasa wa Simba ambao ndiyo wapo wengi uwanjani hapa.

Dakika ya 33: Azam wanafanya shambulizi kali ambapo mpira kutoka kulia unapigwa lakini unakosa mmaliziaji, mchezo ni wa kasi kubwa.

Kikosi cha timu ya Simba.

Dakika ya 30: Simba wanalishambulia kwa kasi lango la Azam.

Dakika ya 16: Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ wa Azam anatolewa kwa kadi nyekundu.

Dakika ya 15: Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ anamchezea faulo Ibrahi, Ajibu wa Simba kwa kumrukia, mwamuzi anamsogelea huku wachezaji wa timu zote wakioneka na kuwa na munkari.

Dakika ya 10: Safu ya kiungo kuna ushindani mkali.

Dakika ya 5: Simba wanaonekana kujipanga na kusogea kwenye lango la Azam mara kadhaa.

Dakika ya kwanza: Mchezo umeanza kwa kasi na timu zote zinasomana.

Timu ndiyo zinaingia uwanjani, Jiji la Dar es Saaam leo kuna mvua maeneo mengi, hata hapa uwanjani kuna mvua inaendelea. Lakini idadi ya mashabiki nao ni wengi kiasi.

Kikosi cha timu ya Azam.

Simba na Azam zinakutana leo kwenye Uwanja wa Taifa katika Kombe la Shirikisho, vikosi vya timu zao, hivi hapa:

Kikosi cha Azam FC kinachoanza dhidi ya Simba SC

1-Aishi Manula

2-Shomary Kapombe

3-Gradiel Michael

4-Daniel Amoah

5-Agrey Morris

6-Stephan Kingue Mpondo

7-Salum Abubakar

8-Himid Mao

9-John Bocco

10-Shabaan Iddi

11-Ramadhan Singano

SUB

-Mwadini Ally

-Erasto Nyoni

-Bruce Kangwa

-Yakubu Mohamed

-Mudathir Yahaya

-Frank Domayo

-Joseph Mahundi

 

KIKOSI CHA SIMBA SC

1-Daniel Agyei

2-Javier Bukungu

3-Mohamed Hussein

4-James Kotei

5-Juuko Murshid

6-Jonas Mkude

7-Shiza Kichuya

8-Mzamiru Yassin

9-Laudit Mavugo

10-Ibrahim Ajibu

11-Mohamed Ibrahim

 

SUB

-Peter Manyika Jr

-Vicent Costa

-Said Ndemla

-Mwinyi Kazimito

-Pastory Athanas

-Juma Luizio

-Fredrick Blagnon

Leave A Reply