The House of Favourite Newspapers

Simba, Ajibu Wamalizana

YANGA SC waliwafanyia umafia Simba kwa kumng’oa Ibrahim Ajibu na kwenda kumtambulisha kwa mbwembwe kisha wakampa uzi wa kijani misimu miwili nyuma.

 

Simba wenyewe walijipoza machungu hayo kwa kumchomoa kiungo fundi Haruna Niyonzima na kumpa jezi nyekundu. Lakini taarifa ikufikie kwamba mara ligi itakapomalizika tu muda wowote Ajibu atarudi kule alikotoka kwa kuvaa tena jezi nyekundu.

 

Vigogo wa Simba wameamua kwani wanataka kuona kombinesheni ya Ajibu na Niyonzima pembeni wakiwa wanawalisha mipira tu washambuliaji wao wakiongozwa na Meddie Kagere. Ishu iliyotufikia mezani ni kwamba tayari Simba wameshamalizana na nahodha huyo wa Yanga na kuna mkataba amesaini lakini ukiwa ni ule wa awali.

 

Nahodha huyo wa Yanga kwa sasa anahesabu tu siku ndani ya klabu yake hiyo kisha achukue virago vyake na kurudi kwao. Waswahili wanasema nyumbani kumenoga. Mkataba wake unafika ukingoni pale msimu huu utakapogota mwishoni.

 

Habari ambazo Championi Jumatatu, limevujishiwa ni kwamba kila kitu juu ya Simba na kiungo huyo mwenye asisti 15 msimu huu kimeenda safi.

“Mkataba wake na Yanga unaisha mwisho wa msimu huu, hivyo kilichofanyika ni kumbeba juu kwa juu kabla mambo hayajawa mengi kwa sasa ndani ya Simba.

 

“Uongozi umeamua kujipanga kuongeza makali ndani ya Simba ili kufanya kikosi kuwa na nguvu na chenye ushindani, sasa njia ya kwanza ni kuwa na wachezaji wenye vipaji kama ilivyo kwa Ajibu,” kilieleza chanzo hicho.

 

Championi Jumatatu lilimbana Meneja wa Ajibu ambaye ni kaka yake, Athuman Ajibu juu ya ishu hiyo na kusema kuwa bado mchezaji wake ana mkataba na Yanga kwa sasa, hivyo itakuwa ngumu kuzungumzia hilo.

 

Ajibu ni mali ya Yanga kwa sasa hivyo siwezi kusema yupo Simba na amesaini huko, hilo ni jambo gumu kulizungumzia,” alisema Athuman.

LUNYAMADZO MLYUKA NA SAID ALLY, Dar

Comments are closed.