The House of Favourite Newspapers

Simba Bingwa wa Mikwaju ya Penati Ligi Kuu Msimu wa 2024/25


Kwenye Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, Simba SC ni timu namba moja kufunga mabao mengi ya penati ndani ya uwanja msimu wa 2024/25.

Rekodi zinaonyesha kuwa Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids baada ya kushuka uwanjani kwenye mechi 25 ikipata ushindi katika mechi 21, sare tatu na kupoteza mchezo mmoja imetupia jumla ya mabao 60.

Kwenye mabao hayo 60 ni mabao 12 yametokana na mikwaju ya penati ambapo Simba SC ilipata jumla ya penati 13 kutokana na faulo ambazo walichezewa ndani ya 18 na wakati mwingine wachezaji wa timu pinzani kushika mpira wakiwa ndani ya 18.

Leonel Ateba mwenye mabao 12 ndani ya ligi huyu anaongoza kupiga penati nyingi ambazo ni 7 katika hizo alifunga sita akikosa moja kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC ni Jonathan Nahimana alikuwa shujaa kwa kuokoa penati hiyo.

Kinara kwenye chati ya utupiaji wa mabao ni Jean Ahoua mwenye mabao 15 katika mabao hayo ni sita kafunga kwa penati na zote kapeleka maumivu kwa makipa kwa kuwa hajakosa penati zote ambazo alipiga na mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.