The House of Favourite Newspapers

Simba Hatari Sana Oktoba Mwanzoni, Yanga Mwishoni

tambweeWachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya mechi.

Nicodemus Jonas,Dar es Salaam
KUELEKEA mtanange wa wababe wa ligi ya Tanzania, Simba na Yanga utakapigwa Jumamosi wikiendi hii, upande wa pili timu hizo zinaingia kukiwa kuna rekodi lukuki nyuma yake, lakini kivutio zaidi ni matokeo ya timu hizo pindi zinapokutana mwezi Oktoba katika michezo ya Ligi Kuu (awali, ilijulikana kama Ligi ya Taifa).

Mchezo wa wikiendi hii, utakuwa wa 82 timu hizo kukutana lakini Yanga wakiwa na takwimu nzuri zaidi, wakiwa wamshinda mara 31 dhidi ya 23 za Simba huku mechi 27 zikitoshana nguvu.

Kwa mujiubu wa takwimu, zinaonyesha timu hizo zimewahi kukutana kila mwezi, yaani kuanzia Januari mpaka Desemba zimewahi kukipiga, lakini tunapozungumzia mechi zilizopigwa Oktoba pekee, timu hizo zimekutana mara 18 na kila moja kushinda mechi sita na sare tano.

Aidha, rekodi zinaonyesha kwenye ushindi huo wa Simba, imekuwa na matokeo mazuri zaidi kwenye tarehe za mwanzo wa mwezi, ambapo imeshinda mechi nne (Oktoba 7, 1979 walishinda 3-1, Oktoba 4, 1980 wakashinda 3-0 na Oktoba 4, 1995 wakashinda 2-1) huku Yanga ikiambulia ushindi mara moja tu Oktoba 9, 1991 waliposhinda mabao 2-0 tu. Kwa maana nyingine Yanga imekuwa na matokeo mazuri inapokuwa katikati ama mwishoni mwa Oktoba.
Kwa mara ya kwanza zilikutana Oktoba 7, 1979 na Simba ikashinda mabao 3-1 na mara ya mwisho takwimu zinaonyesha zilitoshana nguvu ambapo ilikuwa mwaka juzi, Oktoba 18, 2014, ambapo zilisuluhu. Takwimu chini zinajionyesha.
Oktoba 7, 1979: Simba 3-1 Yanga
Oktoba 4, 1980: Simba 3-0 Yanga
Oktoba 20, 1990: Yanga 3-1Simba
Oktoba 9, 1991: Yanga 2-0 Simba
Oktoba 27, 1992: Simba 1-0 Yanga
Oktoba 4, 1995: Simba 2-1 Yanga
Oktoba 29, 2006: Simba 0-0 Yanga
Oktoba 24, 2007: Simba 1-0 Yanga
Oktoba 23,1996: Yanga 1-0 Simba
Oktoba 11,1997: Yanga 1-1 Simba
Oktoba 26, 2008: Simba 0-1 Yanga
Oktoba 31, 2009: Simba 1-0 Yanga
Oktoba 16, 2010: Yanga 1-0 Simba
Oktoba 29, 2011: Yanga 1-0 Simba
Oktoba 3, 2012: Yanga 1-1 Simba
Oktoba 20, 2013: Simba 3-3 Yanga
Oktoba 18, 2014: Simba 0-0 Yanga

Comments are closed.