The House of Favourite Newspapers

Simba: Hiki Chuma Kinachokuja Ni Balaa Zaidi ya Augustine Okrah

0
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally.

BAADA ya kuachana na winga wao wa kimataifa wa Ghana, Augustine Okrah, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amechimba mkwara mzito kuwa wapo kwenye mipango ya kushusha mbadala wa staa huyo mwenye kiwango cha juu.

Uongozi wa Simba juzi Jumatatu ulitangaza rasmi kuachana na Okrah aliyemaliza mkataba wake na Simba kwa kuweka wazi kuwa staa huyo hataongezewa mkataba wa kuendelea kusalia Simba.

Kikosi cha Simba jana Jumanne kilirejea uwanjani kuvaana na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.

Augustine Okrah

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kutangazwa rasmi kufunguliwa kwa dirisha la usajili, Simba katika maboresho ya kikosi chao wanahusishwa na majina makubwa yakiwemo winga wa AS Vita, Erick Kabwe, Yahya Mbegu (Ihefu), Luis Miquissone wa Al Ahly ya Misri sambamba na nyota wa Al Hilal, kipa Issa Fofana na mshambuliaji Makabi Lilepo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ahmed alisema: “Kama ambavyo tumetoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii, tunamshukuru Okrah kwa huduma yake tunaamini ni mchezaji bora lakini kwa kuwa hayupo kwenye mipango ya kocha kwa msimu ujao tulifikia uamuazi wa kuachana naye.

“Uongozi unaendelea kufanya mchakato wa kumalizana na mbadala wake ambaye atakuwa bora zaidi na moto wa kuotea mbali.”

Stori na Joel Thomas na Musa Mateja

MAPYA YAIBUKA, UGOMVI WA GIGY NA BABA LEVO WAFIKA PABAYA,MADOLALI ATIA NENO

 

Leave A Reply