The House of Favourite Newspapers

Simba inamsajili Coutinho

0

coutinhoshangwezagoal.jpg

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesikia kilio cha kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho kutaka kuihama timu yake na amesema anasubiri kauli ya benchi la ufundi ili ampe mkataba.

Hivi karibuni Coutinho raia wa Brazil alinukuliwa akisema hana raha na maisha ya kuwekwa benchi katika kikosi cha Yanga na kusema yupo tayari kuhama hata kwenda Simba ili mradi acheze first eleven.

Hans Poppe aliposikia kauli hiyo ya Coutinho, haraka akaliambia Championi Jumamosi kuwa; “Nimemsikia huyo mchezaji kwamba anataka kuondoka Yanga, sasa mimi nasubiri tu kauli ya benchi la ufundi wakimaliza mzunguko huu wa ligi, wakisema sawa tunamsajili.

“Nadhani hata wao (benchi la ufundi) watakuwa wamesikia kauli ya Coutinho, hivyo kama wakimuweka katika ripoti yao ya usajili hakuna tatizo tunamsajili haraka tu.”

Hans Poppe alisema benchi la ufundi pia litapendekeza nani aachwe ili Coutinho achukue nafasi yake huku pia mpango ukiwa ni kumrejesha Paul Kiongera anayecheza kwa mkopo KCB ya Kenya.

Leave A Reply