The House of Favourite Newspapers

Simba Kuachana Na CEO Wake Imani Kajula

0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula.

Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba Sc imeridhia maombi ya Afisa Mtendaji wake Mkuu, Imani Kajula ya kuomba kuondoka klabuni hapo ifikapo mwisho mwa mwezi Agosti 2024 mkataba wake utakapoisha.

Taarifa ya Wekundu hao wa Msimbazi imebainisha kuwa kufuatia maamuzi hayo, Bodi hiyo inafanya jitihada za kupata Afisa Mtendaji Mkuu mpya na kuongeza kuwa Umma utapewa taarifa zoezi hilo litakapokamilika.

“Pamoja na uamuzi huu, Afisa Mtendaji Mkuu Imani Kajula anaendelea na majukumu yake ya kiutendaji kikamilifu hadi tarehe 31 Agosti 2024.” — Simba Sc.

Leave A Reply