The House of Favourite Newspapers

Simba Kushiriki CAF ni 98% Lakini Yanga Ikifanya Hivi Simba Ndiyo Basi Tena

0
Wachezaji wa timu ya Simba wakipongezana.

Kitendo cha timu ya Simba kufanikiwa kifunga Azam FC bao 1-0 katika Kombe la FA jana, sasa ni imejihakikishia kwa asilimia kubwa nafasi ya kushiriki katika michuano ya kimataifa msimu ujao, ikiwa ni baada ya kupita miaka minne.

Simba inaweza kushiriki katika michuano hiyo ambayo inasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kuwa kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mshindi wa Kombe la FA nchini atawakilisha taifa katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Simba yenyewe imejihakikishia nafasi hiyo licha ya kuwa ndiyo kwanza imefuzu fainali sababu nusu fainali nyingine itazikutanisha Yanga na Mbao FC, leo Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Hivyo, hata kama Simba haitatwaa kombe hilo, katika Ligi Kuu ya Vodacom, bado inaweza kushiriki ikiwa Yanga itaingia fainali ya michuano hiyo pia na kwa kuwa katika ligi kuu timu zinazowania ubingwa ni Yanga na Simba.

Ikiwa Yanga itakuwa bingwa wa ligi kuu na FA, Simba itapata nafasi ya kushiriki kwa kuwa itakuwa imeshika nafasi ya pili FA, ikiwa Simba itatwaa mataji yote basi itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kitu pekee ambacho kinaweza kuinyima Simba nafasi hiyo ni kama Yanga itafungwa na Mbao FC katika nusu fainali kisha Simba ikaja kufungwa kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho na pia ikaukosa ubingwa wa ligi kuu kama utaenda kwa Yanga.

Ikiwa itakuwa hivyo, Yanga itashiriki katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Mbao itashiriki Kombe la Shirikisho.

Timu pekee ambazo zimekuwa zikishiriki katika michuano ya kimataifa inayoandaliwa na CAF ni Yanga na Azam FC kwa miaka minne iliyopita.

Leave A Reply