The House of Favourite Newspapers

Simba Kutotwaa Ubingwa Wa Sportpesa Ni Somo Jingine Tena

WIKIENDI iliyopita timu ya Simba ilichapwa mabao 2-0 na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup iliyofanyoka Nakuru, Kenya.

 

Simba ilishindwa kufurukuta mbele ya wenyeji Gor Mahia ka­tika Uwanja wa Afraha nchini Kenya ilipofanyika michuano hiyo kutokana na kutokuwa vizuri kwenye safu yao ya ushambulia­ji, hivyo kuwapa nafasi wapin­zani wao hao kuibuka na ushindi.

 

Safu ya ushambuliaji ya Simba kiujumla haikuwa nzuri kutoka­na na kuwakosa washambuliaji wake mahiri, John Bocco na Em­manuel Okwi hivyo kusababisha safu hiyo kuwa butu kutokana na kushindwa kufunga bao hata moja tangu michuano ilipoanza hadi walipofikia hatua ya fainali am­bapo walifanikiwa kutinga hatua hiyo kupitia mikwaju ya penalti.

Michuano hii ilikuwa na hamasa kubwa hasa kutokana na kufa­hamika kuwa bingwa wa michuano hiyo anapata nafasi ya kukwea pia kwenda nchini England kucheza mchezo wa kirafiki na Everton.

 

Ukiachana na Simba timu zote za Tanzania ambazo zilishiriki michua­no hiyo, ikiwemo Yanga na Singida United zimeshindwa kufurukuta katika michuano hiyo kutokana na kufanya vibaya ambapo Yanga ilitolewa katika hatua ya kwanza na Singida wakimaliza wa tatu.

 

Inaonyesha wazi kuwa klabu zetu hazijaichukulia michuano hii kwa umakini wa hali ya juu kutokana na matokeo ambayo wameyapata.

 

Yanga na Simba zote zil­ionekana kuwatumia zaidi wache­zaji wapya na wale wa vikosi vya pili hali iliyowafanya watoke mapema kwani wengi wao wal­ionekana hawana uzoefu wala muunganiko kwenye timu husika.

 

Hali hiyo imeonekana kujiru­dia katika michuano ya msimu huu ambapo kikosi cha Simba kimewaacha washambuliaji wake tegemeo ambao ndio walioion­goza timu hiyo kuchukua ub­ingwa kwa kufunga mabao 34 kwa pamoja jambo ambalo si sahihi.

 

Sikatai kwamba Gor Mahia ni timu nzuri na ina ushindani mkubwa, lakini naamini uwepo wa wachezaji hao kungeongeza ushindani zaidi na hata kufani­kiwa kushinda ili kuweza kuipata nafasi ya kwenda nchini England.

 

Kama wachezaji hao walia­chwa kutokana na kuwa majeruhi ambao matatizo yasiyozuilika, hilo halina jinsi hata kidogo ila iwapo waliwaacha tu kwa saba­bu ya kuwapumzisha ili kutu­mia zana mpya haikuwa sahihi kwani uongozi ulipaswa kutam­bua umuhimu wa michuano hiyo kwa kutoibeza hata kidogo.

 

Walitakiwa kuichukulia umakini wa hali ya juu michuano hii ili ku­weza kujiimarisha zaidi kwa kuwa na kikosi imara na si kuifanya mi­chuano hiyo kuwa sehemu ya kupi­mia wachezaji wapya ama wale ambao walikuwa hawapati nafasi.

 

Ikumbukwe kuwa, kupata na­fasi ya kucheza na Everton tena kwao ni sehemu ya kuji­tangaza kwa klabu na nchi kwa ujumla hivyo kuikosa nafasi hiyo ni jambo la kusikitika sana.

 

Kila kukicha tumekuwa tuki­lalamika juu ya soka la Tan­zania kutosonga mbele na badala yake hurudi nyuma kila kukicha hivyo nafasi kama hizi zitumike katika kupiga hatua.

 

Viongozi wanapaswa kujilaumu kwa maamuzi waliyoyafanya ya kutowatumia wachezaji hao am­bao walionyesha kiwango msimu mzima kulikochangia timu kut­waa ubingwa kutokana na ku­chukulia mambo kirahisi rahisi.

Acha Niseme na KHADIJA MNGWAI

Comments are closed.