The House of Favourite Newspapers

Simba Msipotwaa Ubingwa, Tafuteni Sababu Mpya Ya Kuwadanganya Mashabiki

Kikosi cha timu ya Simba.

KATIKA mchezo wa soka duniani kote kila mtu anafahamu kuwa raha ya mechi ni mabao na raha ya ligi ni kumaliza wa kwanza na hatimaye kunyakua ubingwa na si vinginevyo.

 

Hii haina tofauti sana na mchezo wa riadha, maarufu kama mchezo wa kukimbiza upepo ambapo kwa vyovyote vile raha yake ni kumaliza wa kwanza ili upate zawadi ya juu na kujiandikia historia ya kipekee kati­ka mchezo huo dhidi ya washindani wako.

 

Mara nyingi kabla ya msimu mpya wa ligi kuanza viongozi wa klabu huonyesha makucha yao kwa kufanya maandalizi wanayoyaita ‘kabambe’ kwa kuanzia kwenye usa­jili wa wachezaji waliokuwa waki­wawinda kwa muda mrefu.

Si ajabu kwenye zoezi hili la usa­jili kushuhudia sarakasi za kila aina zikiwemo kejeli na hata kutunishi­ana misuli kwa viongozi wa klabu pale inapotokea wote wanamuwania mchezaji mmoja.

 

Vita hivyo ambavyo navifananisha na vile vya panzi, tija kubwa inabaki kwa mchezaji husika kwa kujikuta anajizolea mamilioni ya fedha am­bayo wakati mwingine hayalingani hata kidogo na kiwango alichonacho.

Simba ni miongoni mwa klabu am­bazo viongozi wake huwa hawako­sekani katika purukushani za kugo­mbea mchezaji, lakini msimu huu ndiyo klabu pekee iliyo­tumia kiasi kikubwa cha fedha ku­fanya usajili u n a o t a jwa kuwa ni wa kiwango cha kutisha.

 

Vi o n g o z i wa klabu hiyo kongwe hapa nchini kwa kujiamini ka­bisa tena kwa kifua mbele wame t amk a h a d h a r a n i kwamba usajili wao unafikia kiasi cha shilingi bilioni moja uliofanikisha kuwanasa wachezaji iliokuwa ikiwawinda kwa muda mrefu.

 

Misimu minne imekatika bila Simba kuchukua ubingwa kitendo ambacho siyo tu kinawanyima raha wanachama na mashabiki pekee bali pia hata viongozi wao.

 

Kwa misimu yote hiyo Simba bila ubingwa, viongozi wamekuwa wakikuna vichwa kutafuta sababu za kupoza mioyo ya mashabiki wao ingawa wakati mwingine wali­fanikiwa na kwa vipindi tofauti wakigonga mwamba kuwashaw­ishi kukubaliana na sababu wa­nazozitoa.

 

Kwa mujibu wa viongozi wenyewe wa Simba, huu ndiyo msimu utakaotuliza hasira za mashabiki kwa kukosa ubingwa kwa muda mrefu kwa hicho wa­nachokiamini katika usajili bora walioufanya kuliko hata wapin­zani wao wa jadi, Yanga.

 

Imani hii mliyonayo viongozi wa Simba inapaswa kuendana na vitendo kwa kuhakikisha wachezaji wenu wanaonye­sha kiwango kinacholingana na gharama mliyotumia ku­fanya usajili vinginevyo tafuteni mapema sababu za kuwadanganya mashabiki wenu.

Inafahamika kwamba hakuna jeshi linaloingia vitani likasema linakwenda kushindwa lakini kutoka­na na hali ya ushindani iliyo kwenye ligi hakuna haja ya kutamba kupita kiasi bila kubakiza akiba ya maneno.

STORI: JUMA KATANGA | CHAMPIONI

Comments are closed.