Simba: Salam Ziwafikie

Baada ya usiku wa Januari 13, kufanikiwa kunyakua Kombe la Mapinduzi Cup kule visiwani Zanzibar na kuandika historia kwa kulinyakua kombe hilo kwa mara ya nne.

 

Msemaji wa Mabingwa wapya Ahmed Ally ametamba na kusema huo ni mwanzo kuelekea katika ile mipango yao waliyoipanga ya kunyakua mataji wanayoshiriki msimu huu.

 

Ahmed pia ametumia mwanya huo kuwatumia salamu watani wao wa Jadi yanga kuelekea Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ambako wao ndio mabingwa watetezi.

 

“Timu itasafiri kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wetu na Mbeya City, nawatumia salamu hawa jamaa nao wajipange maana hatutaki mzaha kabisa mwaka huu 2022.

 

“Lengo letu ni kucheza kwa malengo ili mwishoni mwa msimu tutimize tulichokisudia, tumefanikiwa Zanzibar kwa kutwaa Kombe la Mapinduzi, sasa tunaendelea kusaka mataji mengine.” Ahmed Ally- Afisa Habari wa Simba.


Toa comment