Simba SC Shusheni Presha Kidogo

MCHEZAJI wa zamani wa Simba, Seleman Matola ambaye kwa sasa ni kocha wa Lipuli amesema kuwa Simba wakitulia wataishangaza dunia kwenye mchezo wa leo Jumamosi utakaopigwa Lubumbashi.

Simba itacheza mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe nchini wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare mchezo wao wa kwanza Uwanja wa Taifa.

 

Akizungumza na SpotiXtra, Matola alisema kuwa anaona Simba ikipenya hatua ya nusu fainali kutona na namna wachezaji wanavyojituma pamoja na uwezo walionao hivyo wakipunguza papara waliyonayo ni rahisi kwao kupenya.

 

“Naona kuna nafasi kwa Simba kuishangaza dunia kwa sasa kwenye hatua hii kwani namna ambavyo walicheza pale Taifa ni mchezo mkubwa na mbinu nyingi walizitumia hivyo kwa sasa wanachotakiwa kufanya ni kushusha presha.

 

“Suluhu ambayo wameipata sio mbaya sana kwani haijafungwa sasa inachotakiwa kufanya ni kuchanga karata zake vizuri yale makosa ambayo waliyafanya nyuma wayafanyie kazi,” alisema Matola.


Loading...

Toa comment