The House of Favourite Newspapers

Simba SC: TFF Tupeni Yanga FA

Omary Mdose | CHAMPIONI | Dar es Salaam

BAADA ya Simba kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA, kocha msaidizi wa kikosi hicho, Jackson Mayanja, raia wa Uganda, ameibuka na kusema kuwa sasa wanatamani kucheza na Yanga kwenye hatua hiyo.

Simba ambayo Jumapili iliyopita iliifunga Madini FC bao 1-0, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ukiwa ni mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo, imeungana na Mbao FC, huku ikisubiri matokeo ya mechi kati ya Yanga dhidi ya Prisons na Azam dhidi ya Ndanda ili waungane nao hatua ya nusu fainali.

“Tunashukuru kuona mbio zetu za kuelekea kwenye mafanikio msimu huu zinakwenda vizuri, baada ya kutinga nusu fainali, sasa tunasubiri kuona tutacheza dhidi ya nani kwa sababu mechi nyingine za robo fainali bado hazijachezwa.

“Katika nusu fainali, tumejipanga kupambana na timu yoyote ile hata kama itakuwa Yanga itakuwa vizuri zaidi.

“Lakini ikitokea Azam, Mbao au hata nyinginezo, lakini kwanza tusubiri tuone timu hizo nyingine zitafanya nini kwenye michezo yao ya robo fainali,” alisema Mayanja.  

Comments are closed.