Simba SC Wakiwaachia Yanga Dk Ya 80 Wamekufa

Kikosi cha timu ya Simba.

 

YANGA inaonekana kuwa hatari zaidi kufunga mabao yanayowapa pointi kwenye dakika za mwisho pindi inapokutana na Simba kwenye mechi za Ligi Kuu Bara tangu ligi hiyo kuanzishwa kwake.

 

Rekodi hizo zinaonyesha kwamba, kuan­zia dakika ya 80 mpaka 90, Yanga ilipata ushindi mara tatu kufuatia kufunga mabao ndani ya muda huo, huku Simba ikiibuka na ushindi mara moja.

 

Ikumbukwe kuwa, Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana kwenye mchezo wa ligi kuu unaotarajiwa kupigwa Oktoba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

 

Mechi za ushindi za Yanga zipo hivi; Agosti 10, 1974, Yanga 2-1 Simba. Mabao ya Yanga yalifungwa na Gibson Sembuli dakika ya 87 na Sunday Manara (97), huku lile la Simba likifungwa na Adam Sabu (16).

 

Septemba 10, 1983, Yanga 2-0 Simba, ma­bao ya Yanga yalifungwa na Lila Shomari wa Simba aliyejifunga dakika ya 72 na Ahmed Amasha (89). Novemba 8, 1997, Yanga 1-0 Simba, bao lilifungwa na Sekilojo Chambua dakika ya 85. Kwa upande wa Simba, mechi iliyoshinda ilikuwa ni ile ya Septemba 18, 2004, ambapo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Athumani Machuppa dakika ya 82.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Kwa upande wa mechi zilizoisha kwa sare, ilikuwa hivi; Oktoba 11, 1997, Yanga 1-1 Simba, bao la Yanga lilifungwa na Sekilojo Chambua dakika ya 52, Simba ikasawazisha kupitia kwa George Masatu dakika ya 89.

 

Februari 21, 1998, Yanga 1-1 Simba, bao la Yanga lilifungwa na Akida Makunda dakika ya 46, la Simba likafungwa na Athumani Machepe (88). Septemba 30, 2001, Simba 1-1 Yanga, Simba ilianza kufunga kupitia kwa Joseph Kaniki dakika ya 65, Sekilojo Chambua wa Yanga akasawazisha dakika ya 86.

 

Agosti 18, 2002, Simba 1-1 Yanga, bao la Simba lilifungwa na Madaraka Selemani dakika ya 65, lile la Yanga likafungwa na Sekilojo Chambua (89). Oktoba 20, 2013, Simba 3-3 Yanga, Yanga ilianza kufunga kupitia kwa Mrisho Ngassa dakika ya 15, Hamis Kiiza alifunga mawili dakika ya 35 na 45, yale ya Simba yalifungwa na Ditram

 

Mwombeki (53), Joseph Owino (60) na Gilbert Kaze (84).

Aprili 19, 2014, Yanga 1-1 Simba, alianza Haruna Chanongo kuifungia Simba dakika ya 75, kabla ya Simon Msuva hajasawazisha dakika ya 86. Oktoba Mosi, 2016, Yanga 1-1 Simba, Amissi Tambwe aliifungia Yanga dakika ya 26, Shiza Kichuya akasawazisha dakika ya 87. Jumla zimetoka sare mara saba.

Stori: Ibrahim Mussa | Championi Jumatano

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment