The House of Favourite Newspapers

Simba SC Warejea Dar ‘Kuimaliza’ Yanga SC

0
Kotei akisalimiana na mashabiki wa Simba baada ya kuwasili.

Kikosi cha Klabu ya Simba kimemaliza kambi ambayo ilikuwa imewekwa kisiwani Unguja, Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga katika Ngao ya Jamii.

 

Kiungo Said Ndemla akiwasili.

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo timu zote zilikuwa nje ya jiji hilo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo na maandalizi ya msimu wa 2017/18 kwa jumla.

 

Niyonzima akitua.

Wachezaji wa Simba wamewasili Dar es Salaam majira ya saa tano wakiwa na benchi la ufundi baada ya timu hiyo kuwa Unguja kwa siku kadhaa.

 

Wakipanda kwenye basi lao.

Timu hiyo ilirejea Dar kwa ndege na kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kisha kuelekea kambini kujiandaa kwa mchezo huo wa Ngao ya Jamii.

Mkude akiwa na shabiki.

Baadhi ya mastaa waliwasili ni Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Said Ndemla, Kotei, Salim Mbonde na wengine.

Kichuya akirejea.

 

Salim Mbonde akitua.

 

Kocha wa Makipa, Mwarami Mohammed ‘Shilton’ (kushoto) akiambatana na Kocha Msaidizi Jackson Mayanja.

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

 

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Tshishimbi Awapa Wasiwasi Niyonzima,Okwi Baada ya Kuanza ‘Tizi’

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Leave A Reply