The House of Favourite Newspapers

Simba SC Yawapa Mapumziko Wachezaji Wake

0
Kikosi cha cha Simba.

UONGOZI wa Klabu ya Simba umewapa wachezaji wake siku saba za kupumzika baada ya hapo wachezaji hao watarejea kwa ajili ya kujifua ili kujiandaa na mechi za ligi na michuano ile ya kimataifa.

 

Simba inaingia katika mapumziko hayo ikiwa ndi­yo kinara katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 23 baada ya kucheza michezo 11 na inatarajiwa kushiriki mi­chuano ya Kombe la Shirik­isho Afrika.

 

Aki­zungumza na Cham­pioni Juma­tano, Meneja wa klabu hiyo, Richard Rob­ert alisema kwa sasa wametoa mapumziko kwa timu ili watakaporejea waanze kazi rasmi kujiwin­da na michezo ijayo.

 

“Tumetoa mapumziko kwa wachezaji ya siku saba baada ya hapo watare­jea ili kuweza kuende­lea na mazoezi kama mnavyofahamu tuna michuano mbele yetu mikubwa ile ya ligi kuu na Kombe la Shirikisho.

 

“Tutaanza maz­oezi na timu licha ya kwamba wengine watakuwa kwenye michuano ya Cha­lenji lakini tutaendelea mpaka wale wataka­pomaliza na watajiun­ga na timu na lengo ni kufanya vizuri kwa kujikita vizuri katika nafsi ya juu,” alisema Richard.

Stori: Martha Mboma | Championi Jumatano

Leave A Reply