Simba: Tayari Tuna Majina Yote Ya Usajili

MABOSI wa Simba wameweka wazi kwamba licha ya kuwa na majina ya wachezaji ambao wanawahitaji katika msimu ujao lakini kwa sasa wameyaweka pembeni na kutojishughulisha nayo.

 

Mabosi hao wamesema kuwa tayari wana orodha ya wachezaji ambao watawasajili kutoka nje na ndani ya Tanzania, lakini kwa kipindi hiki hawatajishughulisha nao badala yake wanajipa muda wa kuwapitia kabla ya kuwapa mikataba ya kujiunga na timu hiyo.

 

Miongoni mwa majina hayo ni mabeki wawili wa Mtibwa Sugar, Dickson Job na Kibwana Shomary ambao wanatajwa na klabu hiyo kuwa warithi wa nyota Shomary Kapombe na Muivory Coast, Pascal Wawa.

 

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema kuwa tayari wana orodha ya mastaa ambao wanawahitaji kikosini hapo lakini hawako tayari kwa sasa kuanza mchakato huo kutokana na muda wake kutofika.

 

Raia huyo wa Afrika Kusini ameongeza kuwa licha ya kwamba wana majina mengi watafanya usajili maalum ambao utakuwa na lengo la kuziba nafasi wanazozihitaji.

 

“Tuna majina ya wachezaji ambao tunawataka kwa ajili ya msimu ujao baada ya benchi la ufundi kuwasilisha ripoti yao ya nani na nani wanamuhitaji.

 

“Lakini kwa sasa hao wote tumewaacha kwa sababu huu siyo muda wake na pia kwenye orodha hiyo ndefu tutaangalia wale walio bora na watakaokuja kuziba nafasi zile ambazo tutaona zina umuhimu wa kufanya hivyo,” alisema Msauzi huyo.

Stori: Said ally, Dar es Salaam

MOLINGA Amejibu KUONDOKA YANGA – “Tusubiri LIGI Irudi, MPIRA sio KUONGEA ONGEA”


Loading...

Toa comment