Simba: Tunawapiga Berkane

BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba SC, amesema wapinzani wao RS Berkane kwenye mchezo unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumapili hii, hawatatoka salama.

 

Simba inatarajiwa kumenyana na RS Berkane ya Morocco kwenye mchezo wa nne wa Kundi D, wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita ugenini kwa kufungwa mabao 2-0.

 

Barbara amebainisha kuwa, kwa maandalizi ambayo wameyafanya pamoja na kila mchezaji kuhitaji ushindi,

wanaamini wapinzani wao hawatatoka kwa Mkapa.

“Kwa Mkapa hawatoki kwa kuwa maandalizi yapo vizuri na kila mchezaji anajua tunahitaji ushindi. Haya ni mashindano ya kimataifa na tunawakilisha nchi hivyo ni muhimu kwetu kushinda ili kuweza kusonga mbele,” alisema Barbara.

 

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chao, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema: “Maandalizi yetu kuelekea mchezo dhidi ya Berkane yanaendelea vizuri, tunataka kuwatahadharisha Berkane kuwa wamekuja kipindi kibaya kwa kuwa sehemu kubwa ya kikosi chetu wapo salama, tunatarajia kumkosa Chama (Clatous) kutokana na masuala ya kikanuni na Dilunga (Hassan) aliye mgonjwa.”

 

BERKANE KUTUA DAR LEO

Wakati mchezo huo ukitarajiwa kuchezwa Jumapili hii, imefahamika kuwa kikosi cha RS Berkane kipo njiani kuja Tanzania na kinatarajiwa kutua Dar leo Alhamisi majira ya saa nane mchana.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Fiston Abdoul Razak, amesema: “Tumeanza safari leo (jana) ya kuja Tanzania, tunatarajia kufika Dar kesho (Alhamisi) saa nane mchana. Tumetoka Morocco, tumepitia Dubai kuja Tanzania.

 

“Mchezo utakuwa mgumu ila sisi ni bora kuliko Simba, ukiangalia wengine tunapajua na tutahakikisha tunapata matokeo tunayoyataka kwenye mchezo huo.”

 

VIINGILIO

Imeleezwa viingilio vya mchezo huo ni Sh 3000 kwa mzunguko, VIP B na C Sh 20,000, VIP A Sh 30,000 na tiketi za Platinum Sh 150,000.

WAANDISHI WETU, DAR

YANGA WAWAPOKEA TUISILA NA FISTON ABDULRAZACK, RS BERKANE IKITUA AIRPORT DAR KUIVAA SIMBA..

4231
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment