Simba vs Azam Fainali Mapinduzi

KESHO Jumapili katika Uwanja wa Gombani Pemba, Simba itacheza na Azam FC fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya jana Ijumaa timu hizo kushinda mechi zao za nusu fainali zilizochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Unguja. Azam ilikuwa ya kwanza kutinga fainali baada ya kuifunga KMKM mabao 3-0.

 

Mchezo huo ulichezwa saa 10 jioni. Katika mchezo huo, mabao ya Azam yalifungwa na Agrey Morris dakika ya tisa, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ (dk 62) na Obrey Chirwa (dk 82).

Baadaye saa 2 usiku, Simba nayo ikaifunga Malindi kwa penalti 3-1 baada ya dakika tisini kumalizika kwa timu hizo kushindwa kufungana. Katika penalti, wafungaji kwa upande wa Simba ni Yusuph Mlipili, Mohammed Ibrahim na Asante Kwasi, huku Zana Coulibaly akikosa upande wa Simba.

Stori na Kazija Thabit, Zanzibar

Loading...

Toa comment