The House of Favourite Newspapers

SIMBA WAANZA MIKAKATI YA KUIMALIZA SEVILLA

SIMBA watatumia fursa waliyopata kucheza na timu maarufu ya La Liga, Sevilla kuwapa uzoefu wa kimataifa wachezaji wake. Simba itacheza na Sevilla Mei 23 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku timu hiyo ya Hispania itawasili nchini Mei 21 chini ya udhamini wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa Tanzania.

 

Ofi sa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa mbali ya kutotwaa ubingwa wa SportPesa, lakini wameweza kufanya vizuri zaidi kulinganisha na timu zote na uteuzi wao utaongeza ushindani katika mashindano hayo SportPesa.

 

“Simba kwa sasa ipo katika kiwango cha juu na kucheza na Sevilla itasaidia kujua viwango vya wachezaji wao katika mechi za kimataifa, husasani timu zinazotoka bara la Ulaya,” alisema Manara. “Mechi hii inaiweka Tanzania katika historia kubwa sana katika soka.

 

Historia zinaonyesha kuwa miaka ya nyuma, timu mbalimbali kutoka nje ya mipaka ya Afrika zilikuja hapa Tanzania na kucheza na Yanga na Simba, miaka ya hivi karibuni hakukuwa na ujio huo zaidi ya mwaka 2017 ambapo SportPesa iliileta timu ya Everton na kucheza timu ya Gor Mahia ya Kenya.

 

“Nawapongeza SportPesa kwa kufanya mambo haya ambayo yanachangia maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania. Timu kama Aston Villa na timu maarufu za Brazili, Norway zilikuwa zinakuja nchini na kucheza mechi na klabu zetu,” alisema

Na:WILBERT MOLANDI,

Comments are closed.