The House of Favourite Newspapers

Simba Wachemka kwa Gadiel Michael

MABOSI wapya wa Yanga wamefanikisha mipango ya kumuongezea mkataba wa miaka mitatu beki wake, Gadiel
Michael ambaye ilikuwa kiduchu tu asaini Simba.

 

Dau alilowekewa mezani beki huyo lilikuwa ni Shilingi Milioni 40 na mshahara wa Milioni tatu. Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra halina wasiwasi wowote nazo ni kwamba beki huyo wamefikia makubaliano na viongozi wa timu hiyo na wamemhakikishia mambo mazuri yanakuja akae mkao wa kula.

 

Mmoja wa viongozi wa Yanga, Fredrick Mwakalebela licha ya kutoweka wazi lakini alisisitiza kwamba kila kitu freshi Wanayanga watulie wanasuka chama la maana.

Gadiel ni miongoni mwa wachezaji wenye umri mdogo waliofanya vizuri na Yanga msimu uliopita. Habari zinasema kwamba Simba walishamseti lakini akawaambia ataendelea kubaki Yanga

Comments are closed.