The House of Favourite Newspapers

Simba Wafanya Dua Maalumu Ya Kumwombea Mo Dewji (Picha + Video)

Klabu ya Simba leo imefanya dua ya kumuombea mwekezaji wake mkuu, Mohammed Dewji ‘Mo’ ambaye jana alfajiri alitekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni raia wa kigeni.

 

 

Tukio hilo lilitokea katika Hotel ya Colosseum wakati alipokuwa akienda kufanya mazoezi katika Gym iliyopo hotelini hapo.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanachama wa Simba wakiongozwa na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Dalali wamefanya dua ya kumuombea Mo ili aweze kuwa salama huko aliko lakini pia aweze kuungana na familia yake akiwa salama bila ya tatizo lolote.

Dua hiyo imefanyika, makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo mpaka sasa bado hali ya mambo ni tata isipokuwa jeshi la polisi nchini linaendelea na harakati zake za kuhakikisha Mo anapatikana lakini pia wahusika wa tukio hilo wanatiwa mbaroni.

PICHA/HABARI: SWEETBERT LUKONGE | GPL

Comments are closed.