The House of Favourite Newspapers

Simba waichapa Kagera Sugar 3-1

0

kiiza

TIMU ya Simba SC leo imeibuka kifua mbele baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao yote ya Wekundu wa Msimbazi yamewekwa kimiani na mshambuliaji raia wa Uganda, Hamis Kiiza aliyepiga ‘hat trick’ na kuondoka na mpira wake baada ya mechi.

Bao pekee la Kagera Sugar limefungwa na Mbarak Yusuf.

Kwa matokeo ya leo, Simba wamefikisha jumla ya pointi 9 wakiwa wamecheza michezo mitatu.

Leave A Reply