Kartra

Simba Waipigia Hesabu Ruvu

LICHA ya jana Jumamosi kuwa na mchezo mgumu ugenini dhidi ya Namungo FC, lakini akili za Simba zipo kwenye mchezo ujao dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

 

Ikumbukwe kwamba, mchezo wa kwanza walipocheza Uwanja wa Uhuru, Dar, ubao ulisoma Simba 0-1 Ruvu Shooting jambo ambalo limewafanya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kufikiria namna ya kulipa kisasi.

 

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, aliliambia Spoti Xtra kuwa, kila mchezo kwao ni muhimu kushinda ili kufikia malengo yao jambo linalowafanya wawe na hesabu kali kila wanaposhuka dimbani.

 

“Tuna mechi nyingi za kucheza kwa sasa, hivyo kila mchezo tunaufikiria na tunajua kwamba tukimaliza mchezo mmoja unafuata mwingine ambao unakuwa mgumu zaidi, hivyo yote tunakwenda nayo sawa.

 

“Kikubwa ambacho tunahitaji ni ushindi kwani tayari tumefanikisha lengo la kwanza la kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, kinachofuata ni mechi zetu ambazo zipo ndani ya ligi, mashabiki watupe sapoti,” alisema Gomes.

 

Juni 3, mwaka huu, Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA, SPOTI XTRA


Toa comment