The House of Favourite Newspapers

Simba Waitumia Prisons Kuisogelea Yanga SC

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes raia wa Ufaransa, amefunguka kwamba, anataka kuitumia mechi yao ya kesho Jumatano dhidi ya Prisons kwa ajili ya kuwasogelea wapinzani wake, Yanga.

 

Mfaransa huyo ameongeza kwamba, mechi hiyo pia ataitumia kwa ajili ya kuongeza presha kwa wapinzani wake Yanga ambao ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara hadi sasa.

 

Simba, kesho Jumatano watakuwa wenyeji wa Prisons katika mechi ya ligi kuu ambayo itapigwa Uwanja wa Mkapa, Dar. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa, Prisons waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

“Kwa sasa akili yetu ni juu ya mechi ya Jumatano dhidi ya Prisons, hii ni muhimu kwetu kwa sababu tunataka kuwapa presha Yanga ambao wapo juu yetu.“

 

Tukishinda tutakuwa karibu yao zaidi na hii itakuwa nzuri kwetu, muhimu tutacheza tukiwa tunajua ni kitu gani ambacho tutakuwa tunakitaka,” alimaliza Gomes.

 

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba wapo nafasi ya pili wakikusanya pointi 45 baada ya kucheza mechi 19, huku Yanga wakiongoza na pointi 50 na mechi zao 23.

 

Wakati Simba na Prisons wakienda kupambana, takwimu zinaonyesha kwamba, washambuliaji wawili wa Simba, John Bocco na Chris Mugalu, idadi yao ya mabao ni sawa na ile iliyofungwa na timu nzima ya Prisons katika ligi kuu msimu huu.

 

Bocco mwenye mabao tisa na Mugalu matano, jumla yake ni 14 ambayo ndiyo yamefungwa na timu nzima ya Prisons msimu huu huku kinara wao akiwa Jumanne Elfadhili mwenye matatu.

STORI: SAID ALLY NA LUNYAMADZO MLYUKA

Leave A Reply