The House of Favourite Newspapers

Simba walivyowavamia Wakongo kishujaa

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa kikosi chake kipo imara kuwavaa AS Vita na wanatua kishujaa jijini Kinshasa na hawana wasiwasi hata chembe. Simba watamenyana na AS Vita ya Congo, Jumamosi saa moja jioni, ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa wakiwa na kumbukumbu ya kuanza kwa ushindi mbele ya JS Saoura ya Algeria huku wapinzani wao wakiwa na maumivu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili, Aussems amesema anawatambua wapinzani wake kwa kuwa alipata muda wa kuifuatilia timu hiyo na amegundua ni timu bora haipaswi kubezwa wao wanaifuata kishujaa.

 

“Tumeanza vizuri ina maana morali ya wachezaji ni kubwa, kazi yetu iliyo mbele yetu ni kuona tunafikia malengo kwa kupata matokeo pia kwenye mchezo wetu wa ugenini bila kuwa na hofu yoyote, hilo linawezekana.

 

“Kipaumbele kwa wachezaji wangu ni kuona tunapata matokeo kwenye mchezo wetu kwa hali na mali, hali ambayo imenifanya niwape wachezaji mbinu kali zitakazotufanya tupate matokeo, nimewaambia wachezaji nataka mabao ya mapema ili kufanikiwa kuumudu mchezo,” alisema Aussems.

 

Simba wanatarajia kuondoka nchini leo asubuhi kuwafuata wapinzani wao AS Vita ambao wapo nao kundi D ambalo kwa sasa Simba anaongoza kwa kuwa na idadi ya mabao matatu akifuatiwa na Al Ahly ambao wana mabao matatu, As Vita na JS Saoura hazina pointi.

 

“Kila mchezaji wangu ndani ya timu ana thamani sawa na mchezaji mwingine hivyo kukosekana kwa mchezaji mmoja ama wawili kwangu ni pigo ambalo linanifanya nisiwe na furaha ila haimaanishi ni sababu ya kushindwa kupata matokeo. Wachezaji ambao atawakosa John Bocco, Erasto Nyoni na Shomari Kapombe ambaye naye pia anatibu mguu wake.

LUNYAMADZO MLYUKA

Comments are closed.