Simba Wapangua Fitina za Wazambia Wakiwa Dar

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try again’, amesema kuwa wanazijua
mbinu na fitina zote za soka la
Afrika, hivyo hawana mashaka na mchezo wa marudiano dhidi ya Red Arrows.


Try Again alifunguka
kwamba wanakwenda Zambia wakiwa kama wanajeshi na kila kitu kuhusu mchezo
huo kimekaa sawa, hakuna
jambo lolote au figisu yoyote watakayofanyiwa na wasiijue.

 

Simba wanatarajia kusafiri kesho Jumamosi kwenda Lusaka, Zambia kucheza mchezo wa marejeano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi Red Arrows. Mchezo huo utachezwa, keshokutwa Jumapili.


Akizungumzia mikakati
na uwezekano wa kufanyiwa figisu wakiwa ugenini, Try alisema: “Simba ni timu
kubwa sana, inajua kila mbinu
za soka la Afrika. Kwa hiyo haiwezi kutusumbua kabisa.


“Tunakwenda na mbinu ya
kivita kwenye mchezo huo na Wanasimba wote niwaambie tu, tunakwenda kufanya
vizuri kwenye mechi hiyo
kwa sababu tuna kocha na wachezaji bora.”

STORI NA ISSA LIPONDA, Dar es Salaam3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment