The House of Favourite Newspapers

Simba Watamba Kufuzu Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos

0
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba.

UONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa, mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos, ni muhimu kufanikisha malengo ya kutinga hatua makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo uliopita ugeni, ubao ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba, hivyo Jumapili hii wakiwa wanarudiana, Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote, au sare ya bao 1-1 kushuka chini ili ifuzu.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, ameweka wazi kuwa watatumia Uwanja wa Azam Complex kukamilisha kazi ya kufuzu hatua ya makundi.

“Tunawakabili Power Dynamos Uwanja wa Azam Complex ambao tutautumia kufuzu hatua ya makundi, mechi itakuwa saa 10 jioni kwa kuwa michezo mingi tulicheza kwenye muda huo.

“Kikosi leo (jana) kimefanya mazoezi Uwanja wa Azam Complex kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wengi wanaoujua uwanja ule na wengine hawaujui.

“Viingilio ni rafiki pia kwenye mchezo kama huu, msimu uliopita tuliingiza watu 47,000, lakini sasa tutakuwa na mashabiki 7,000. Mashabiki wanaotaka kuwepo uwanjani wanunue tiketi mapema. Tiketi za mzunguko ni Sh 10,000, VIP B Sh 30,000 na Platinum Sh 150,000.

“Wachezaji watatu watakosekana kwenye huo mchezo ambao ni Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo.

“Power Dynamos wanatarajiwa kuwasili nchini kesho (leo) Alhamisi majira ya saa 12 jioni na Shirika la Ndege la ATCL. Waamuzi wanatarajia kufika Tanzania tarehe 30 Septemba,” alisema Ally.

MWANDISHI WETU – SPOTI XTRA

Leave A Reply