The House of Favourite Newspapers

Simba Watamba Kuifunga Ruvu Shooting Kirumba Leo

0

KOCHAMsaidizi wa Simba, Seleman Matola, amesema pamoja na ugumu wanaokutana nao katika kusaka pointi kutokana na kukamiwa na wapinzani wao, lakini suala la timu yao kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu ni la lazima.

 

Kauli ya kocha huyo imekuja ikiwa leo Alhamisi Simba itapambana na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa ukiwa ni mwendelezo wa ligi hiyo.

 

Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 64 baada ya kucheza mechi 26, wanafuatiwa na Yanga wenye pointi 61 na Azam 60.

Matola ameliambia Spoti Xtra kwamba: “Timu nyingi tunazocheza nazo zipo katika hatari ya kushuka daraja ndiyo maana mechi hizo zinakuwa ngumu kwetu, lakini pamoja na kukamiwa huko, sisi tumejiandaa kuhakikisha kila mchezo ulio mbele yetu tunashinda ili tutwae ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo.

“Sio kazi rahisi kwetu kutetea ubingwa kwa msimu wa nne, lakini tutafanya kila liwezekanalo ili kutimiza malengo hayo tukianza na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.”

Stori: Johnson James, Mwanza

Leave A Reply