The House of Favourite Newspapers

Simba Watibua Usajili Yanga SC

SIKU chache baada ya kuwepo tetesi za Yanga kumuwania kinara wa mabao wa Ligi Kuu Bara, Eliud Ambokile katika usajili wa dirisha dogo ambalo linafunguliwa katikati ya mwezi ujao, watani wao wa jadi Simba nao wameibuka kuiwania saini ya nyota huyo.

Ambokile hivi sasa anaongoza kwenye ufun­gaji kwenye Ligi Kuu Bara, akiwa amepachika mabao sita katika msimu huu wa ligi akifuatiwa na Habib Kyombo wa Singida United mwenye matano.

Yanga inataka kumsa­jili Ambokile kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Mkongoman, Heritier Makambo pamoja na Ibra­him Ajibu.

Lakini taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata, nikwamba Simba imeingilia usajili wa Ambokile kwa ajili ya kuiongozea nguvu safu yao ya ushambuliaji inayoon­

 gozwa na Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na John Bocco ambayo kwa mechi za hivi karibuni imeshindwa kuonyesha makali.

 

Mtoa taarifa wetu alisema, Simba wanataka kumsa­jili Ambokile kwa ajili ya kumtumia kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji anaye­tokea pembeni namba 7 au 11 nafasi ambazo Ambokile anazimudu zote.

Aliongeza kuwa, katika mahitaji ya kocha anataka kiungo mshambuliaji mwenye kasi atakayeanzisha mashambulizi kutokea pembeni, sifa ambayo anayo Ambokile.

“Timu inahi­taji kiungo msham­buliaji mwenye kasi atakayeanzisha mashambulizi kwa maana ya kupiga krosi na kufunga mabao, atakayesa­jiliwa katika usajili wa dirisha dogo.

 

“Na tayari majina ya baadhi ya wachezaji yameanza kupendekezwa na kati ya hayo yupo mshambuliaji Ambokile anayeichezea Mbeya City na kama mambo yakienda vizuri basi tutamsajili,” al­isema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Ambokile kuzungumzia hilo alisema: “Zipo baadhi ya timu zilizonifuata kwa ajili ya kufanya nazo mazungumzo ili nisaini mkataba, katika usajili wa dirisha dogo.

 

“Nisingependa kuziweka wazi kwa hivi sasa hizo timu zilizonifuata ambazo ni klabu kubwa hapa nchini tayari nimeziam­bia nimebakiza mkataba wa miezi sita, hivyo ziifuate timu yangu ya Mbeya City kwa ajili ya kufanya nayo maz­ungumzo kabla ya kunifuata mimi, kama unavyofaha­mu sheria za soka.”

Ambokile amesema anataka shilingi milioni 40 ili asaini mkataba.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam  

MSIKIE KOCHA WA STARS AKIFUNGUKA HAPA KILICHOTOKEA

Mechi za leo hizi hapa, bashiri na Biko ushinde mkwanja chapchap, bofya hapa ==> BIKO SPORTS

Comments are closed.