The House of Favourite Newspapers

Simba Watua ‘Kibabe’ jijini Mwanza, Ruvu Wajipange (Picha +Video)

0

KIKOSI cha Simba SC leo Juni 1, 2021 kimewasili jijini Mwanza kujiandaa na mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Ruvu Shooting unatarajiwa kuchezwa Juni 3, 2021 katika Uwanja wa CCM kirumba uliopo jijini Mwanza.

Kikosi Cha Simba kimetua kikiwa na jumla ya wachezaji 21,  akizungumza baada ya kufika katika Uwanja wa ndege wa Mwanza Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwani timu katika michezo yake yote popote inapocheza hapa nchini ni nyumbani kwa hiyo Simba haina michezo ya ugenini wala nyumbani michezo yote ikicheza ipo nyumbani hivyo kupata matokeo ni lazima.

 

Kwa upende wao baadhi ya mashabiki ambao wamekuja kuipokea Simba wamesema wao wamejiandaa kuisapoti kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanapata matokeo katika michezo watakayocheza.

Leave A Reply