The House of Favourite Newspapers

SIMBA YAENDELEA KULA VIPORO, YAISHUSHA AZAM FC NAFASI YA PILI

EMMANUEL Okwi anarejea kwenye ubora wake jana baada ya kufunga bao moja kati ya mabao 2-1 waliyoshinda leo mbele ya KMC uwanja wa CCM Kirumba.

Okwi alifunga bao hilo dakika ya 23 akimalizia pasi ya James Kotei na kuizamisha moja kwa moja kimiani, kipindi cha pili.
Hili inakuwa ni bao la tatu kwa Okwi akifunga mfululizo, alianza mbele ya Kagera Sugar akafunga pia mbele ya Alliance na leo mbele ya KMC na anafikisha jumla ya mabao 10.
 KMC walizidisha ushambulizi na kusawazisha dakika ya 57 lililopachikwa kiufundi na Hassan Kabunda akitumia makosa ya beki wa kupanda na kushuka Zana Coulibary.
Licha ya KMC kufanya mashambulizi mengi kupitia upande wa Zana bado walishindwa kupata bao la pili.
 Dakika ya 75 Simba walipopata penalti baada ya mchezaji wa KMC kuunawa ndani ya 18 penalti ambayo ilidakwa na Jonathan Nahimana kwa kumzidi ujanja Kagere ambaye staili yake ya kushtua iligunduliwa.
Dakika saba mbele Mzamiru Yassin akatengeneza penalti nyingine na mwamuzi wa mchezo, Kambuzi akaamua kutoa penalti kwa Simba iliyopigwa na nahodha John Bocco dakika ya 82.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 66 akijikita nafasi ya pili kwa idadi ya mabao ambayo anayo kibindoni tofauti na Azam FC.
Simba wamefunga jumla ya mabao 53 huku Azam FC wakiwa na mabao 49 kibindon kwa sasa.
Kituo kinachofuata kwa Simba ni dhidi ya Biashara United utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Karume.

Comments are closed.