The House of Favourite Newspapers

SIMBA YAENDELEZA UBABE, YAZIDI KUJIHAKIKISHIA UBINGWA

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wameeneleza ubabe na kuishushia kipigo cha bao 2-0 Klabu ya Tanzania Prisons.

Simba wameendelea kutopoteza mchezo kwenye ligi msimu huu baada ya kuiadhibu Prison kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam jioni hii.

 

Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 35 na Emmanuel Okwi kwa njia ya penati dakika ya 80. Bocco anafikisha mabao 14 ya Ligi Kuu msimu huu huku Okwi akifikisha mabao 19.

 

 

Simba sasa imefikisha pointi 58 katika michezo 24 ya ligi msimu huu hivyo kuendelea kujikita kileleni ikiwakimbia wapinzani wao Yanga ambao wapo katika nafasi ya pili wakiwa na alama 47.

 

Simba iko mbele ya Yanga kwa michezo miwili ambapo Yanga inayowakilisha taifa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho imecheza mechi 22 pekee hivyo ikishinda viporo vyake inaweza kufikisha alama 53.

Comments are closed.