The House of Favourite Newspapers

SIMBA YAHAMISHIA MAZOEZI GYMCANA – VIDEO

KLABU ya Simba mapema leo imeamua kuhamishia mazoezi yake kwenye Uwanja wa GYMCANA Posta jijini Dar es Salaam, ikiwa ni harakati moja wapo ya kuhakikisha inajinoa vizuri kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya watani wao  wa Jadi Yanga.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa eshokutwa, Jumapili, Septemba 30 Mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tangu wajichimbie kwenye kambi yake iliyopo katika fukwe za Mbezi kwenye Hoteli ya  Seascape, Simba ilikuwa ikifanyia mazoezi yake kwenye Uwanja wa Boko Veterani, lakini kadri homa ya mpambano huo inavyozidi kushamiri wameamua kuhamishia mazoezi yao kwenye Uwanja wa GYMCANA ambapo mapema leo wamefanyia.

 

Stori: Musa  Mateja

BALAA Kikosi cha Simba Kilivyojifua Kuiliza Yanga

Comments are closed.