SIMBA YAICHANA YANGA, YADAI IMEWAPOTEZA KWENYE MAPATO

UONGOZI wa Simba umesema kuwa umewapoteza kwa mbali wapinzani wao kwenye mahesabu pamoja na mashabiki waliohudhuria kwenye mechi za kimataifa za kirafiki.

 

Yanga ilianza Jumapili kucheza na Kariobangs Sharks uwanja wa Taifa na ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 kabla ya Simba kumalizia Jumanne na Power Dynamo ambapo ilishinda mabao 3-1 uwanja wa Taifa.

 

Haji Manara , Ofisa Habari wa Simba amesema,: “Tunaposema Simba ni klabu ya watu muwe mnaelewa
idadi ya watu 48,630 (Kwa Yanga), mapato milioni 283.

“Champion (mabingwa ambao ni Simba) idadi ya watu 58,001,mapato, milioni 376 na chenji kibao. Hapo ndio game yao ilikuwa na matangazo mwezi mzima hadi maandamano na mabango mitaani.

 

“Simba tumetumia only three days (siku tatu) za promotions na game yetu ilikuwa working day (siku ya kazi) Jumanne ,” amesema.


Loading...

Toa comment