The House of Favourite Newspapers

Simba Yaingia Mkataba wa Miaka Mitatu na Serengeti Breweries (SBL) – Video

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti ​Breweries Limited, Obinna Anyalebechi (kushoto) akipewa jezi na CEO Simba, Imani Kajula 

Timu ya Simba imeingia mkataba wa udhamini wa miaka mitatu kati ya Simba SC na Serengeti Breweries Limited (SBL) kupitia kinywaji chake cha Pilsner Lager ukisainiwa.

CEO Simba SC, Imani Kajula amesema “Ni ubia wa nguvu kabisa, ubia wa Simba wawili, hii ni package ambayo imekuja wakati mwafaka, Serengeti ni Mbia mkubwa sana wa mpira wa Tanzania, huu ni mendelezo wa kusaidia mpira”

“Hili ni tukio la kihistoria. Katika mechi zote ambazo Simba inacheza mtaani kunanona na naamini Pilsner Lager kuwa mshirika wa Simba hata mauzo yataongezeka. Mashabiki wa Simba wanapenda kujipa raha. Tunaamini ushirikiano huu utazidi kutujenga. Tunawaahidi kupitia Simba bia itakuwa maarufu zaidi.”- Mjumbe wa Bodi, Raphael Chegeni.

“Tunajivunia kuziunganisha taasisi mbili kubwa za SBL na Simba kwa mkataba wa udhamini wa miaka mitatu. Kupitia udhamini huu utaifanya bia yetu ya Pilsner Lager kuwa mdhamini wa Simba.”

“Udhamini huu utakuwa na thamani ya Tsh. 1.5 bilioni. Kwa udhamini huu tunaamini utasaidia kukuza michezo nchini kwetu. Simama Imara, Songa Mbele Kama Simba.”- Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti ​Breweries Limited, Obinna Anyalebechi.

SIMBA HAWAPOI, HAMASA KUELEKEA DERBY na YANGA USIPIME, AHMED ALLY ATANGAZA VITA….

Leave A Reply