testiingg
The House of Favourite Newspapers

Simba Yaipiga Vipers ya Uganda Kwa Mkapa, Clatous Chama Apangua Safu ya Ulinzi

0

ILIWABIDI Simba wasubiri hadi dakika ya 45 wapate bao la pekee kupitia kwa  ambaye aliipangua safu ya ulinzi ya Vipers na kuweka mpira wavuni.

Hiyo ilitokea jana usiku pale Dimba la Mkapa katika mchezo wa raundi ya nne ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji Simba dhidi ya Vipers ya Uganda na wenyeji wakashinda bao 1-0.

Mchezo huo wa Kundi C ulianza kwa timu zote kufanya mashambulizi ya kuviziana ambapo Simba kupitia kwa Pape Osman Sakho walikosa mabao dakika ya nne na sita halikadhalika Vipers nao walifanya mashambulizi wakimtumia Setam Yunus yaliokolewa na kipa Aishi Manula.

Ni dakika ya 45 Chama aliingia na mpira kwenye boksi kisha akampiga chenga beki wa Vipers na kupiga shuti ambalo lilimpita kipa na kuzama nyavuni. Simba walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao hilo moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Simba wakitafuta bao la kuongeza wakati Vipers wakihitaji kusawazisha.

Dakika ya 69 Chama almanusura afunge bao la pili kwa Simba baada ya kumpiga chenga kipa wa Vipers krosi yake iliokolewa na Livingstone Mulondo.

Vipers walifanya shambulizi la hatari dakika za mwisho lakini Manula alisimama imara langoni mwake na kuokoa shuti hilo lililopigwa na Martin Kizza.

Kwa ushindi huo, sasa Simba wanakwea hadi nafasi ya pili wakiwa na alama sita baada ya kucheza michezo minne, kinara akiwa Raja Casablanca ambao jana waliwababua Horoya AC mabao 3-1 kule Guinea.

ORUMA – “KOCHA ROBERTINHO APEWE MIEZI MITATU SIMBA, HESABU za RAJA ZIMEISHA”…

Leave A Reply