Simba Yaishushia Mvua ya Magoli Coastal, Yaipiga 7-0

MABINGWA watetezi wa Ligi kuu Bara, Simba leo Novemba 21 imeshusha kipigo kizito msimu huu, baada ya kuichapa Coastal Union kwa mabao 7-0 mchezo uliochezwa kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha.

 

Kiungo Hassan Dilunga ndiye alifungua karamu ya mabao akifunga bao  la mapema kabisa dakika ya 7 ya mchezo.

 

Katika Mchezo huo Nahodha John Bocco alifanikiwa kufunga magoli matatu (Hat-trick)  kwenye dakika ya 25,29 na dakika ya 38.

 

Baada ya kumaliza adahabu ya kufungiwa mechi tatu Bernard Morrison amerejea vizuri akifanikiwa kuiandikia Simba  bao dakika 45 na kuiweka mbele kwa magoli 5-0 mpaka mapumnziko.

 

Clautus Chama aliingia kambani mara mbili dakika ya 60 na 85 akifunga goli kali kwa mpira wa adhabu akihitimisha mvua hiyo ya mabao kwa Simba.

 

Baada ya Ushindi wa leo Wekundu wa Msimbazi wamefikisha pointi 24 wakiwa kwenye nafasi ya tatu, pamoja na kipigo cha leo kutyoka kwa KMC, timu ya Azam wanaongoza ligi kwa muda wakiwa na alama 25 hadi kesho kwani endapo Yanga wenye alama 24 wakishinda dhidi ya Namungo wataongoza msimamo wa ligi.

 

Toa comment