The House of Favourite Newspapers

Simba Yaitungua Gwambina, Yapaa Kileleni

0

BINGWA mtetezi wa ligi Kuu Tanzania bara Simba  imefanikiwa kukwea kwenye kileleni kwenye msimamo wa wa ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gwabina Fc, katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Gwambina , Misungwi Mwanza.

 

Goli pekee la Mnyama Simba limefungwa na beki wa kushoto Mohamed Hussein ‘Zimbwe’ dakika ya 29 kwa mkwaju wa mbali uliomshinda mlinda mlango wa Gwambina Mohamed Makaka.

 

Akizungumza baada ya mechi Zimbwe amesema licha ya uwanja kuwa mbovu wamejitahidi kutengeneza nafasi na wamefanikiwa kupata ushindi.

 

Kwa matokeo hayo sasa ni rasmi Simba inaishusha Yanga katika nafasi ya kwanza baada ya kufikisha alama 58 baada ya kushuka dimbani mara 24, na Yanga wapo nafasi ya pili na alama 57 baada ya mechi  26.

 

Keshi ligi hiyo itaendelea kwa Yanga kucheza na  Azam Fc kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam

 

Leave A Reply