Kartra

Simba Yaitungua KMC 2-0, Yanusa Ubingwa

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Bara Simba , imefanikiwa kuondoka na alama tatu dhidi ya KMC baada ya kuicharaza kwa mabao 2-0, katika mchezo uliochezwa jana usiku Julai 7,  Uwanja  wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

 

Mabao ya Chris Mugalu dakika ya 2’ na 44’ yalitosha kuipa pointi tatu Simba ambayo ilitoka kupoteza mchezo wake uliopita kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga.

 

Katika mchezo huo Beki wao Andrew Vincent alitolewa kipindi cha pili kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.

 

Simba imefunga jumla ya mabao 71 huku Yanga ikiwa imefunga jumla ya mabao 50 imecheza mechi 32 na imebakiza mechi mbili wakati Simba imecheza mechi 31 na imebakiza mechi tatu.

 

.

Sasa Simba inafikisha pointi 76 ikiwa na uhakika wa kutwaa ubingwa wao kwa kuwa pointi hizo zinaweza kufikiwa na Yanga ila tatizo itakuwa katika idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa, KMC inabaki nafasi ya sita na pointi 42 baada ya kucheza jumla ya mechi 32 ndani ya ligi.

 


Toa comment