The House of Favourite Newspapers

Simba yampa Mavugo Sh milioni 100

0

mavugo-agiye-kugaruka-muri-kiyovu-_53f3764f70777 Straika wa Vital’O ya Burundi, Laudit Mavugo.

SIMBA haitaki mchezo kabisa katika kujenga kikosi chake, kwani imetenga kiasi cha dau la dola 50,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 100 ili iweze kumsajili straika wa Vital’O ya Burundi, Laudit Mavugo.

http://www.ruhagoyacu.com/local/cache-vignettes/L600xH581/Laudit-3159e.jpg

Laudit Mavugo (kushoto) akifanya yake.

Nguvu yote hiyo imewekwa na Simba kuhakikisha Mavugo anatua kikosini kwao aungane na Hamis Kiiza kuipa nguvu safu ya ushambuliaji ya timu hiyo iliyofunga mabao 15 hadi sasa.

Awali kabla ya kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Simba ilimtaka Mavugo na kumtangulizia dola 10,000 lakini uongozi wa Vital’O uliweka ngumu ukitaka dola 100,000 ili umuachie straika huyo na dili likaishia hapo.

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya Simba, uongozi wa klabu hiyo chini ya Rais Evans Aveva, upo tayari kutoa dola 50,000 ili Mavugo asajiliwe na si zaidi ya hapo kwani ndiyo uwezo wa timu kwa sasa.

“Kama asipotufanyia uhuni, basi tutamsajili lakini akileta tamaa ya fedha tutamwachia aende zake, ila kusema kweli tunamuhitaji na tayari tumeshaanza naye mazungumzo,” kilisema chanzo hicho.

Simba ina uhakika ikimpata Mavugo na kiungo mshambuliaji Raphael Kiongera inayemrejesha kutoka KCB ya Kenya, basi itakuwa na kikosi bora katika ligi.

Alipoulizwa Aveva kuhusiana na mpango huo, alisema: “Ni kweli kabisa tuna mpango wa kumsajili Mavugo, ila kuhusu hizo fedha ni nani aliyewaeleza? Nyie tambueni tunamtaka Mavugo.”

Hata hivyo, Mavugo amebakiwa na miezi mitano tu katika mkataba wake na sasa anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote ila kuhusu kusajiliwa ni hadi klabu yake ikubali kuvunja mkataba. Kamati ya Usajili ya Simba iliyo chini ya Mwenyekiti, Zacharia Hans Pope ndiyo yenye maamuzi ya mwisho ya usajili.

 

 

Leave A Reply