Simba Yampeleka Gym Kibu Denis

BAADA ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Simba, aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya City, Kibu Denis, ameanza programu maalum ya mazoezi ya gym kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea msimu ujao wa 2021/22.


Inaelezwa kuwa, tayari Kibu
amekamilisha kila kitu na Simba kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao, na sasa anasubiri kutambulishwa rasmi kama ambavyo wachezaji wengine wapya wa kikosi hicho walivyofanyiwa.

 

Kibu amesajiliwa Simba kama pendekezo la Kocha Mkuu, Didier Gomes ambapo anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, ambayo inatajwa iko kwenye mpango wa kuachana na straika mmoja.

 

Akiwa na Mbeya City msimu uliopita, Kibu alionesha uwezo mzuri kiasi cha kuhusika kwenye zaidi ya mabao manne, na kupata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi, Juni, mwaka huu.Kuhusu usajili wake, Kibu aliliambia Spoti Xtra kwamba: “Nipo Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha usajili wangu kwenye klabu moja kubwa, tuendelee kusubiri kila kitu kitawekwa wazi hivi karibuni.”


Toa comment