Simba Yamsajili wa kiungo Omari Omari kutoka Mashujaa
Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Omari Omari kutoka Mashujaa FC kwa mkataba wa miaka miwili.
Omari ni mchezaji kijana mwenye umri wa miaka 19 ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi tofauti Uwanjani. Omari anaweza kucheza kwa ufasaha namba 8, 10, 11 na 7.