Simba Yamshusha Kiboko Ya Mkude

MBABANE Swallows wamethibi­tisha nia ya Simba kumsainisha kiungo wao tegemeo, Njabulo Ndlo­vu kabla ya dirisha dogo kufungwa Jumamosi.

 

Simba inataka kumsajili mchezaji huyo ili kuima­risha safu ya kiungo kwavile Kocha Patrick Aussems amemuelewa mavitu yake.

 

Ingawa Swallows wamethibitisha kupitia ukurasa wao wa Facebook jana Juma­tano lakini habari kutoka ndani ya Simba zinasema kwamba ni chaguo la Aussems.

Habari zinasema kwamba Aussems ame­vutiwa na uchezaji wa Nd­lovu ambaye anadhani ni mchezaji sahihi wa kumpa changamoto Jonas Mkude kwenye kiungo cha Simba.

 

Simba ingawa wana mechi ngumu dhidi ya Nka­na Jumamosi jijini Kitwe, Zambia lakini vigogo wen­gine wanaendelea na harakati za kumaliza dili la Ndlovu kwani usajili utamalizika Jumamosi hiyohi­yo wakiwa ugenini kabla dirisha hali­jafungwa

Loading...

Toa comment